
658 views
Mheshimwa Johnson Muthama alikuwa mgeni wetu asubuhi ya leo, Alhamisi, 6, Oktoba 2016 na baadhi ya aliyozungumzia, moja ilikuwa suala la muungano wa CORD ambao wengi wadai kuwa kuna msukosuko, huku viongozi wa ODM, Wiper na Ford Kenya; Raila Odinga, Kalonzo Musyoka na Moses Wetangula mtawalia wakinukuliwa katika mikutano ya hadhara wakijipigia upato kupeperusha bendera ya CORD. Huku akiwa mwanachama wa Wiper, Muthama ambaye ni seneta wa Machakos alikiri kuwa licha ya chenye wengi wamekuwa wakishuhudia au wanayoamini, muungano wa CORD uko imara na kuwa ni hali ya kufurahia demokrasia.