
1,869 views
Mbali na kufahamika kwa nyimbo zake za injili na msisimko wake wa kupendeza, ni dhahiri kuwa Size 8 ana talanta chungu nzima kwani kando ya hayo yote, msanii huyu aliyevuma kwa nyimbo kama 'Mateke' 'Ni Yesu' na 'Tam Tam' ana wingi wa hekima, kipawa ambacho anatumia kushauri kinadada. Size 8 ambaye alizaliwa, Linet Masiro Munyali alizuru studio za Radio Jambo Ijumaa, tarehe 30, Novemba 2016 ambapo licha ya kuzungumzia maswala ya usanii na maisha yake, alichukua fursa hiyo kushauri wana ndoa, haswa wanawake.