
1,101 views
Gavana wa Bomet, Isaac Rutto alizuru studio za Radio Jambo siku ya Jumatatu, 26/9/2016 ambapo alizungumzia maswala mengi ya kisiasa na maendeleo swala moja likiwa la minofu ya 'nyama' ambayo rais Uhuru Kenyatta alikiri kuwa serikali ya Jubilee inafurahia. Gavana Rutto ambaye amekuwa kwenye vyombo vya habari kwa maswala mengi, mojawapo ikiwa uhusiano wake na naibu wa rais, William Ruto, maoni yake kuhusu uongozi wa Jubilee na pia chama chake kijulikanacho kama 'Chama Cha Mashinani' ambacho anasema kuwa kimahusika na na mambo yanayowakumba wananchi wa kawaida.