
2,279 views
Leo kwenye kipindi cha Gidi na Ghost Asubuhi, mwanasiasa Kalembe Ndile alizuru stesheni yetu na licha ya kuchambua siasa za humu nchini, kama kawaida ama kama ilivyo ada yake, aliwacha wenyeji wake na maumivu chungu nzima kwenye mbavu zao kwa kicheko si haba. Mheshimiwa Ndile ambaye ni miungoni mwa wanasiasa wacheshi zaidi nchini, hakuwacha mbwembwe na pia sarakasi zake katika mda wake studioni, huku ikiwa mara ya pili kwake kuzuru. Mara ya mwisho Ndile kuzuru ilikuwa mwaka uliopita pindi tu alipoteuliwa mwanachama wa bodi ya mamlaka ya kusimamia huduma za maji Kenya.