
2,296 views
Ni nadra sana kupata habari au maelezo kuhusu mwana au wana ambao wameangaza kwa hisani ya vipawa au vipaji vyao, haswa wana wa chini ya umri miaka mitano. Basi leo tunamuangazia Jaaziah, ambaye ni mwawanawe mtangazaji wa Radio Jambo, Justus Mwakideu kijana mtanashati aliye na kipawa cha uimbaji huku akiwa na umri wa mwaka mmoja na miezi sita tu!. Jaaziah aliwashangaza sana mashabiki wake Mwakideu ambaye ni mtangazaji wa kipindi cha Jambo Mawiu, kipindi cha injili ambacho huja kwako kuanzia mida ya saa kumi na mbili hadi saa nne asubuhi kila Jumapili.