
7,208 views
Jumanne asubuhi, wanajambo walishuhudia kisanga kimoja wakti wa kipindi cha patanisho ambapo Jamaa kwa jina, Patrick alipo omba apatanishwe na mkewe Peninah ambaye walikuwa wamekosana masaa ishirini na manne tu. Kisa na maana; Patrick alikuwa amefika nyumbani akiwa amechelewa. Kulingana na Patrick, alikuwa ameelekea kutizama mechi ya mpira mtaani kwao ambapo alichelewa. Kabla ya kufika nyumbani kwao, rafikiye mmoja alimwomba aelekee kwake ili akawapatanishe yeye na mkewe. Patanisho ndani ya patanisho.