
392 views
Wenyeji wa mji wa Mbale kaunti ya vihiga hapo jana walishuhudia kioja cha bure baada ya mzee wa umri wa miaka 68 kwa jina David Abisai kutoka kijiji cha Visiru kata ya Wamuluma kupashwa tohara mbele ya umati wa watu. Iligundulika kuwa mzee huyo hakuwa amepashwa tohara muda huu wote baada ya kumpiga mkewe ambaye aliwataarufu mangariba na tangu mangariba hao wamekuwa wakimtafuta na hatimaye kupatikana Jumatatu.