
149 views
Mwaka uliopita, gavana wa Bungoma Kenneth Lusaka aliishangaza dunia baada ya kutangaza kuwa kaunti yake imenunua toroli tisa ambazo ziligarimu takriban shilingi laki moja na kumi. (Ksh109,000). Huku akizungumza katika mahojiano yake na watangazaji, Gidi na Ghost asubuhi ya Jumatano, Lusaka alifafanua kuwa toroli hizo zilikuwa zitumike katika kichinjio kipya kabisa cha Chwele ambacho kitakuwa kinatumika kuchinjia kuku ambazo zitakuwa zauzwa hadi nje ya nchi.