
512 views
Huku siasa za kaunti ya Nairobi zikiendelea kupamba moto, mbunge wa eneo bunge la Starehe, Maina Kamanda alitoa sauti yake kuhusu swala hili, huku ikizingatiwa kuwa hivi maajuzi, wabunge saba wa mrengo wa Jubilee walimwidhinisha waziri wa maji Eugene Wamalwa kuwania kiti cha ugavana jijini Nairobi katika uchaguzi mkuu ujao.