
460 views
Kama ilivyo ada yake, Ghost Mulee kila asubuhi kuanzia mida ya saa kumi na mbili asubuhi hadi saa nne, uhondo, mbwembwe na kukuru kakara zinazoendelea dunia amini usiamini, haziwezi mpita yeye kama kiranja mkuu. Siku ya Ijumaa, bwana Ghost alisimulia kisa cha kuhuzunisha ambacho kilitokea maeneo ya Kapeguria mjini ambapo mwanamke mmoja mpangaji alizushiwa na mwenye nyumba kwa madai kuwa wenzake ambao pia ni wapangaji, walilalamika kuwa wanao kumi na wawili wana kelele chungu nzima.