
10,879 views
Yusuf Juma anayetambulika kwa jina la utani kama 'YJ', anatambulika zaidi miongoni mwa mashabiki wa Radio Jambo kwa sauti ya kina huku wengi wao wakiisifia kama sauti iliyo na uwezo wa kutoa nyoka pangoni. Licha ya kusoma habari kila baada ya saa na nusu saa kila siku ya wiki, kutoka mida ya saa kumina mbili hadi saa nne, mwanahabari huyu wa miraba minne pia ana kitengo cha 'Kiswahili sio mdomo wetu'. Kupitia kitengo hiki, zaidi ya wakenya millioni 10 hupata fursa ya kujifunza maneno au majina mapya ya Swahili. Lakini je, ni yepi haswa huendelea wakti wa usomaji habari?. Kupitia mtandao wake wa Youtube YUSUF JUMA-KENYA bwana YJ alijibu swali hilo baada ya kuchapisha kanda yake, huku akionesha ubabe wake nyuma ya kipaza sauti,.