
3,619 views
kanda inayoonyesha maspika wa bunge, Justin Muturi wa bunge kuu na Ekwe Ethuro wa seneti wakisakata ngoma na kucheza twisti imeibuka mitandaoni na kupata umaarufu mkuu. Kanda hii ya dakika mbili yamwonyesha spika Ekwe Ethuro akiwatumbuiza waheshimiwa wenza huku akiuimba wimbo maarufu wa "Taxi Driver" , wake mwendazake Daudi Kabaka. Dakika chache baadaye, spika wa bunge la taifa, Justin Muturi anajiunga naye Ethuro kwenye jukwaa huku akiwashangaza wengi kwa ujuzi na umaahiri wake wa kusakata ngoma kwa mtindo wa twisti.