
275 views
Kwa hakika, ukistaajabu ya Musa utayaona ya firauni. Wakaazi wa kijiji cha Sinoko eneo bunge la Webuye mashariki wameachwa vinywa wazi baada ya mzee mmoja eneo hilo kudai kwamba jogoo wake ni wa umri wa miaka 27. Majirani na wakoo wa Andrew Chiuli wamedai kwamba jogoo huyo alirithiwa kutoka kwa mzee wa boma hilo Christopher Chiuli aliyefariki mwaka wa 2005. Chiuli amedai kwamba jogoo huyo ambaye ni wa buheri wa afya, hula chakula cha kawaida na ni kama Baraka katika boma hilo na hata liweje hawezi kumchinja hadi atakapo aga dunia mwenyewe.