
1,201 views
"Nitajie tajiri mmoja duniani aliyetajirika kwa kucheza bahati nasibu". Hilo ndilo lilikuwa changamoto la Gidi kwa wasikilizaji asubuhi ya leo, alipokuwa akizungumzia swala la bahati nasibu na jinsi limekita mizizi humu nchini huku akichambua mbivu na mbichi kuhusu mchezo wa bahati nasibu. Mjadala huo ulizuka wakati Gidi alipokuwa akiyachambua magazeti na kupata makala moja ambapo mtu mmoja mtaani Eastleigh, aliwauwa mameneja wawili wa casino moja jijini Nairobi baada ya kupoteza shilingi 30,000 kwa mchezo wa bahati nasibu.