
34 views
Kufuatia madai ya ufisadi dhidi ya Sam Nyamweya, Ghost Mulee aliyekuwa mkufunzi wa timu ya kitaifa alipendekeza kuwa ingekuwa jambo la busara kama rais wa shirikisho la FKF, Sam Nyamweya angejiuzulu ili kuwapatia wapelelezi nafasi murwa ya kufanya uchunguzi dhidi ya madai hayo ya ufisadi. Huku akielezea hayo, Ghost Mulee alitaja mifano kadhaa ambayo inaashiria shida ambazo zinaikumba timu ya taifa Harambee Stars huku misingi yake ikiwa swala la ufisadi.