
113 views
Wakizungumzia taarifa hii na zingine, mtangazaji Gidi alielezea wenzake Jacob Ghost Mulee na Yusuf Juma kuwa kati ya mashabiki wa Radio Jambo walitilia shaka taarifa hiyo, wakishikilia kuwa hakuna vile Kenya ingekosa kuorodheshwa kama taifa fisadi zaidi. Msikilizaji mmoja pia alitilia mkazo kuwa huenda ripoti hiyo ikakosa ukweli fulani kwani ufisadi umekithiri nchini, na basi ni bayana kwamba Kenya ndio nchi fisadi zaidi barani Afrika.