
2,178 views
Juhudi ya Gidi na Ghost na kupatanisha mwanaume mmoja na bibi yake siku ya leo iligonga mwamba baada ya mwanaume huyo kupokea simu akiwa gerezani. Ni wazi kwamba mwanaume huyo amepitia masaibu si haba baada ya bibi wake wa miaka nne kumwacha mwezi moja iliyopita kwa sababu ya yeye kuwa mlevi kupindukia. Kufuatia hayo mwanaume alitaka kujitia kitanzi lakini akaamua vingine baada ya kununua kamba. Aliamua kuokoa ndoa kwa kutafuta usaidizi wa Gidi na Ghost na hivyo basi alituma ujumbe Radio Jambo akiomba asaidiwe apatanishwe na bibiye. Hata hivyo alipopigwa simu na Gidi na Ghost, maskini wa Mungu alipokea simu akiwa gerezani na akajuza Gidi na Ghost kuwa yeye ni taniboy na amekamatwa na polisi kwa sababu alikuwa anakosa stakabadhi muhimu.