
2,762 views
Katika kitengo cha leo cha Patanisho, Lyn alitaka usaidizi wa Ghost na Bramwell ili apatanishwe na dada yake Queen. Lyn anadai kuwa walikosana dada yake baada ya kugundua kuwa Queen aliingia katika uhusiano wa kimapenzi na mpenzi wake wa zamani mpaka wakaoana. Lyn hakufurahishwa na jambo hilo na kufikia siku ya leo, hakuwa ameongea na dada wake wa kipekee kwa muda wa mwaka mzima.