
97 views
Katika Makala ya Jasho Langu Riziki Yangu, riziki haiji kwa njia moja. Kwa wengine ni biashara, kwa wengine ni kilimo, na kwa wengine ni kazi ya mikono inayohitaji nguvu, uvumilivu na moyo wa kutokata tamaa. Leo hii tunamwangazia mama Sarah Naomi Sifuna, mwenye umri wa miaka 61, mkazi wa Kijiji cha Yuya kwenye Kaunti ya Trans-nzoia, ambaye kwa miaka 15 sasa amekuwa akitengeneza matofali. Imekuwa sehemu ya safari yake ya kutafuta maisha kupitia jasho lake mwenyewe. Edited & Uploaded by Razaq Malik Graphics by John Muthui ©2025 Radio47 Cape Media Limited