
41 views
Katika mahojiano na Tracy Andiwo, Mtaalamu wa Elimu ya Msingi, tunaangazia umuhimu wa elimu jumuishi kwa watoto wenye ulemavu, changamoto wanazokumbana nazo shuleni na nafasi ya walimu katika kuwasaidia. Anasisitiza pia umuhimu wa kuwapa wazazi na walezi mafunzo kuhusu utunzaji wa watoto wenye ulemavu, pamoja na hitaji la walimu kupata mafunzo maalum ili kuwapa watoto hawa elimu na msaada unaofaa.