
74 views
Katika mahojiano haya, Tabitha Mutinda anazungumzia uongozi, uwakilishi wa kijinsia na nafasi ya wanawake katika uongozi. Anaeleza umuhimu wa viongozi kuwa tayari kutumikia wananchi wakati wowote, huku akisisitiza uwajibikaji, kujitolea na umuhimu wa wanawake kusaidiana na kuinuana katika nafasi za uongozi. Pia anatoa mtazamo wake kuhusu kanuni ya 2/3 ya uwakilishi wa kijinsia na changamoto zinazozunguka utekelezaji wake nchini.