
153 views
Riziki Ojiambo, mchambuzi wa masuala ya kisiasa, anaeleza kuwa kuondoka kwa kiongozi mwenye ushawishi kama Raila Odinga kunaweza kuibua mvutano kuhusu urithi wa kisiasa na mwelekeo wa uongozi. Akizungumzia hali ya siasa baada ya kifo cha Raila, Ojiambo anasema vuta nikuvute inaweza kujitokeza wakati makundi na viongozi wanapojaribu kujipanga upya na kuamua nani atachukua nafasi katika mustakabali wa kisiasa.