
234 views
Dr. Peter Mbae amesema DCP inatarajia kumuidhinisha Rigathi Gachagua kuwa mgombea wake wa Urais katika Mkutano Mkuu wa Kitaifa wa chama hicho mwezi Novemba. Mbae alisema hatua hiyo itafuatiwa na mazungumzo na vyama vingine vya upinzani kuhusu mgombea wa pamoja wa uchaguzi wa 2027.