
52 views
Shebah ni mwanabiashara aliyeamua kutumia kipaji chake cha urembo kama chanzo cha kujipatia kipato. Bila kusomea taaluma hii rasmi, ameendeleza ujuzi wake kupitia mazoezi, kujifunza na kujituma. Leo, anajishughulisha na kusuka nywele na kutengeneza kucha, huku akijenga jina na wateja wake kupitia referrals na mitandao ya kijamii. Anaamini kuwa kipaji kikipewa bidii na nidhamu, kinaweza kuwa chanzo cha mafanikio na kujitegemea.