
22 views
Shule zinafunguliwa Agosti 24, huku wazazi wengi wakikabiliana na changamoto za kifedha katika maandalizi ya muhula mpya. Rais William Ruto amesema serikali imetuma KSh bilioni 18 kwa shule, lakini baadhi ya walimu wakuu wanadai kuwa fedha hizo bado hazijafika. Je, fedha hizo zilitumwa kweli? Ziko wapi, na kwa nini baadhi ya shule zinasema hazijazipokea? Katika video hii, tunachambua madai haya na hali halisi inayowakabili wazazi na shule wakati wa kufunguliwa kwa shule.