
3,255 views
Kuripotiwa kwa ugonjwa wa ukimwi miaka ya themanini, kuliwaacha wengi vinywa wazi. Watafiti wakakuna vichwa wakijaribu kubaini chanzo cha ugonjwa huo ambao kabla ya kugunduliwa kwa dawa za kupunguza makali, wengi wao walipungukiwa uzani kwa kiwango kikubwa, hivyo kuogofya na kutengwa na wanajamii. Licha ya harakati tele za kupiga vita unyanyapaa na dhuluma dhidi ya waathiriwa, kundi la akina mama linadai kupitia masaibu tele. Wanadai kulazimishwa kufanyiwa oparesheni na madaktari kwa lengo la kuwazuia kushika mimba ili kuzuia kuenea kwa madhara ya ugonjwa huo kwa wanao. Jambo la kusikitisha ni kwamba wanafanyiwa hivyo na madaktari waliohitimu na kufunzwa madili ya taaluma hiyo, bila wenyewe kufahamu. Beatrice Maganga amesema na baadhi yao wanaoelezea masikitiko waliyo nayo na kuandaa makala, KILIO CHA HAKI. Created with http://tovid.io