
162 views
Naibu rais William Ruto amesisitiza kuwa chama cha Jubilee hakina mgombea anayependelewa kuliko mwengine. Aidha Ruto amesema kuwa uchaguzi wa chama utafanyika kuwateua watakaopeperusha bendera ya chama. Haya yanajiri huku wasiwasi ukitanda chamani kufuatia madai kwamba baadhi ya wagombea akiwemo waziri wa maji Eugene Wamalwa wanadekezwa.