
59 views
Timu ya taifa ya kandanda harambee stars hapo kesho itachuana na taifa stars ya tanzania kwenye mechi ya kirafiki ambayo itasakatwa katika uwanja wa kasarani. Mechi hiyo ni mojawapo ya mechi ambazo kenya itatumia kujiandaa kwa mechi ya kufuzu kombe la afrika dhidi ya Congo tarehe tano mwezi Juni. Nahodha Victor Wanyama alijiunga na timu hiyo hii leo na yeye ni miongoni mwa wachezaji ambao wanachezea vilabu vya nje ambao wanatarajiwa kucheza mechi hiyo.