
90 views
Seneta wa Kakamega Boni Khalwale alifikishwa katika mahakama moja mjini kakamega akikabiliwa na tuhuma ya kusababisha vurugu. Khalwale ambaye alikuwa ameandamana na seneta wa Bungoma Moses Wetang’ula alikamatwa kwa kuongoza maandamano dhidi ya tume ya IEBC mjini humo. Hata hivyo khalwale hakujibu mashtaka mawakili wake wakidai kuwa tuhuma hizo zina nia ya kumdhuru. Upande wa mashtaka ulisisitiza kuwa tuhuma hizo zilikuwa sawa na pia kwamba kuna uwezekano wa khalwale kufunguliwa mashtakazaidi. Hakimu atatoa uamuzi Ijumaa ijayo ikiwa ni tarehe 3 juni.