
27 views
Viongozi kina Mama nchini wameeleza hofu yao kuhusu mzozo kati ya IEBC na CORD na kuitisha kikomo kwa makabiliano na ghasia. Wanataka majadiliano na njia zingine za amani kutumika kusuluhisha mizozo ya siasa nchini. Kina mama hawajasazwa kwenye makabiliano maandamanoni, baadhi yao wakipata majeraha ya risasi na viboko.