
50 views
Kampuni ya mawasaliano nchini Safaricom hii leo imezindua awamu ya nne ya msururu wa mashindano ya mbio nchini. Kampuni hiyo vilevile imetoa ufadhili wa shillingi millioni 80 kwa mashindano hayo. Kampuni hiyo pia imedokeza kwamba itafadhili mashindano ya mchujo ambayo yatatumika kuchagua timu ambayo itaiwakilisha kenya katika mashindano ya olimpiki mwezi agosti jijini rio nchini brazil.mkondo wa kwanza wa msururu wa mashindano ya humu nchini utaandaliwa tarehe 26 hadi tarehe 28 mwezi Mei.