
154 views
Muungano wa CORD umeilaumu serikali kwa kile umekitaja kuwa kutumia nguvu za kupita kiasi dhidi ya waandamanaji… wakuu wa CORD Raila Odinga, Kalonzo Musyoka na Moses Wetangula wamesema raia wana haki ya kuandamana kuelezea hisia zao kuhusu maswala wasiyoyapenda. Viongozi hao wa upinzaniw amezungumza muda mfupi baada ya kutimuliwa kwa vitoza machozi eneo la kati ya jiji. Wakati huo huo chama cha TNA kimesema ari ya muungano wa CORD ya kuendeleza maandamano nchini yanafaa kuongozwa na sheria badala ya mihemuko. Katibu mkuu wa chama cha tna Onyango Oloo amepuuza mpango wa CORD wa kuandaa maandamano kila jumatatu akisema kwamba katiba inatoa maelezo kuhusu njia ya kuwaondoa maafisa wa tume huru ya uchaguzi na mipaka afisini.