
96 views
Wakati huo huo chama cha TNA kimesema ari ya muungano wa CORD ya kuendeleza maandamano nchini yanafaa kuongozwa na sheria badala ya mihemuko. Katibu mkuu wa chama cha tna onyango oloo amepuuza mpango wa CORD wa kuandaa maandamano kila jumatatu akisema kwamba katiba inatoa maelezo kuhusu njia ya kuwaondoa maafisa wa tume huru ya uchaguzi na mipaka afisini.