
49 views
Katibu mkuu wa muungano wa wafanyikazi nchini COTU, Francis Atwoli amechaguliwa kwa muhula mwnegine wa nne mfululizo ili kuuongoza muungano huo. Atwoli na wenzake 32 walichaguliwa bila kupingwa katika uchaguzi uliofanyika huko Kisumu na kuhudhuriwa na maafisa wa leba kutoka mataifa mbalimbali. Kabla ya kuchaguliwa kwake Atwoli aliwataka maafisa wa polisi kukoma kutumia nguvu kwa waandamanaji wa CORD. Naye kiongozi wa ANC Musalia Mudavadi alisema suala la IEBC halitakiwi kupuuzwa.