
334 views
Askofu wa jimbo la angalikana la Kericho Jackson Ole Sapit sasa ndiye mkuu mpya wa kanisa la anglikana nchini. Ole Sapit amechaguliwa adhuhuri ya leo kwenye uchaguzi wa faragha katika makao makuu ya angalikana nchini All Saints Cathedral jijini Nairobi. Askofu sapit anatarajiwa kuchukua mahala pake askofu mkuu wa sasa Eliud Wabukala ambaye anastaafu mwezi ujao. Nick Wambua anaarifu.