
28 views
Bunge litakua na kikao maalum siku ya Alhamisi tarehe 26 mwezi May kwa ajili ya kujadili mswada wa kukabili utumizi wa madawa ya kusisimua misuli, hii ni baada ya shirikisho linakabiliana na utumizi wa madawa WADA kutaja Kenya kama nchi ambayo haikuafikiana na matakwa yake. Mwezi uliopita rais Uhuru Kenyatta aliweka saini kuupitisha tayari mswada ule ulioidhinishwa na wada kupitia kwa shirikisho la Kenya linalopiga vita utumizi wa dawa za kutitimua misuli Adak.