
27 views
Kikosi cha Kenya cha Raga ya kina dada ya wachezaji saba kitakachoshiriki katika msururu wa raga ulimwenguni mkondo wa Ufaransa kimetajwa. Kikosi hicho kinajumuisha Sinaida Aura ambaye anarejea kikosini baada ya kuuguza jeraha. Chini ya ukufunzi wa Mike Shamia kina dada hao wana ari ya kufanya vizuri huku wakijiandaa kwa mashindano ya Olimpiki.