
125 views
John Osogo alifika mbele ya jopo linalomchunguza jaji wa mahakama ya juu zaidi Phillip Tunoi na kukana kiapo alichoandika Geofrey Kiplagat Lelmet. Osogo ambaye ni msaidizi wa Gavana wa Nairobi Evans Kidero, alimtaja Lelmet kama mwanahabari anayependa kuomba pesa kando na kusema hajawaji kukaa mkao naye na Micheal Njeru kuhusiana na sakata wala kufanya mahojiano ya simu kati yake na jaji Phillip Tunoi. Hata hivyo Osogo alikuwa na kibarua kigumu kuelezea ni kwanini Kiplagat akaamua kuwataja yeye na mfanyibiashara Michela Njeru. Kiplagat anatazamiwa kurudi tena kufafanua yalitojitokeza kwenye kikao cha leo.