Abdul Nondo: 'Watekaji wamenionya niongee nikiongea wataniua'

  • | BBC Swahili
    8,606 views
    “Walinifunga kitambaa cheusi kwenye macho, kamba mikononi … walinisafirisha kwa mwendo huku nikipigwa na baadaye walininginiza mahali, miguu juu huku wakinipiga kwenye unyao wa miguu, walinipiga mgongo na mikononi,” - Mwanasiasa wa chama cha upinzani Tanzania ACT Wazalendo, Abdul Nondo ameieleza BBC huku akisema watekaji walikuwa wakimpa vitisho kila mara. - Nondo ambaye ni Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana ya ACT Wazalengo, amedai kuwa alikamatwa na kuchukuliwa kwa nguvu na watu sita dakika chache baada ya kuwasili katika eneo la Stendi Kuu ya Mabasi jijini Dar es Salaam akitokea Kigoma alipokuwepo kikazi. Sikiliza yaliyomsibu kama alivyomsimulia mwandishi wetu Halima Nyanza. Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw