- 243 viewsKatika Kaunti ya Trans Nzoia, abiria walilazimika kupiga kambi katika Kituo cha Magari mjini Kitale baada ya kituo hicho kusalia mahame, hali iliyosababisha huduma za uchukuzi kulemazwa kwa muda. Wameipa serikali muda wa kushusha bei ya mafuta wakisema gharama ya juu ya mafuta ndiyo chanzo cha usumbufu huo na kusambaratika kwa huduma za usafiri.