Afande Sele: Soko la muziki limekuwa rahisi, laini na limetanuka

  • | BBC Swahili
    627 views
    Msanii mkongwe wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania Selemani Msindi almaarufu kama Afande Sele amesema hawezi kurudi kwenye siasa tena kutokana na kile anachokiita kutokuwepo kwa ukweli. @afandesele1976 alivuma na vibao kama Watu pori, Darubini kali na vingine vingi ambavyo vilimzolea umaarufu mkubwa hata kutwaa tuzo ya mfalme wa Rhymes jina ambalo limesalia kwake hadi hii leo. Lakini siku za hivi karibuni amewekeza nguvu zake kwenye utoaji elimu ya utunzaji wa mazingira kupitia muziki, makongamano na hata bustani darasa nyumbani kwake aliyoipa jina la Pori la Simba @eagansalla_gifted_sounds alimtembelea Mkoani Morogoro na kuandaa taarifa hii. #bbcswahili #tanzania #morogoro Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw