Afisa wa polisi Alex Charo, aliyejeruhiwa vibaya hadi kupofuka baada ya kuvamiwa aomba msaada

  • | Citizen TV
    1,356 views

    Maafisa wa polisi hutekeleza majukumu muhimu sana ya kudumisha sheria na utangamano. Kazi yao huwaweka kwenye hatari ya kuvamiwa kama ilivyofanyika kwa Alex Charo aliyejeruhiwa vibaya hadi kupofuka. Na kama anavyoarifu Roba Liban, afisa huyo wa zamani wa polisi ameishi maisha ya uchochole tangu alipopoteza uwezo wa kuona alipojeruhiwa akiwa kazini huko Marereni kaunti ya Kilifi.