Afisa wa polisi Fredrick Leliman ahukumiwa kifo kwa mauaji ya wakili Willie Kimani

  • | Citizen TV
    1,595 views

    Mahakama imemhukumu aliyekuwa afisa wa polisi ambaye pia ni mhusika mkuu kwenye mauaji ya wakili willie kimani , Fredrick Leliman, Kifo.aidha aliyekuwa afisa wa polisi Stephen Cheburet amefungwa miaka 30 gerezani huku mshtakiwa wa tatu Sylvia Wanjiku akifungwa miaka 24 gerezani. aliyekuwa akitoa habari kwa polisi Peter Ngugi amefungw amiaka 20 gerezani. wanatuhumiwa kumuua wakili Willie Kimani, mteja wake Josephat Mwenda na dereva Joseph Muiruri. watatu hao waliuwawa mwaka 2016 na maiti yao kutupwa mtoni old donyo sabuk.