Afisa wa usalama barabarani wa Iraq aeleza masaibu ya joto kali

  • | BBC Swahili
    Iraq ni mojawapo ya maeneo yenye mazingira magumu zaidi duniani inapokuja katika suala la hali ya hewa . Kuangalia jinsi Wairaq wanavyokabiliana na mabadiliko ya hali ya juu ya tabia nchi, Msimu wa vipindi vya BBC vya maisha katika nyuzijoto 50- BBC’s Life At 50 uliamua kumfuata askari wa usalama barabarani katika mji mkuu Baghdad wakati alipokuwa akifanya kazi katika hali ya hewa ya nyuzijoto zaidi ya 50. Na tunasikia pia kutoka kwa mkulima ambaye anapambana kuendelea na maisha yake katika hali ngumu ya hewa inayotishia kuangamiza mimea yake. #bbcswahili #iraq #mazingira