Skip to main content
Skip to main content

Afisi ya Naibu Rais inapendekeza bajeti ya ziada ya Sh1.8 bilioni

  • | Citizen TV
    1,181 views
    Duration: 2:53
    Afisi ya Naibu Rais Profesa Kithure Kindiki imependekeza bajeti ya ziada ya shilingi bilioni 1.8. Katibu katika afisi hiyo, Moses Mbaruku, amesema kuwa pesa hizo ni za matumizi ya ofisi, mishahara, usafiri na maandalizi ya hafla mbalimbali. Aidha, Mbaruku amekanusha madai ya matumizi ya shilingi milioni 44 na afisi ya mkewe Naibu Rais, akisema kwamba mdhibiti wa bajeti alitoa taarifa hiyo kimakosa kwani afisi hiyo ilifutwa mbali.