Ajali katika barabara kuu ya Nakuru - Kisumu yaua mtu mmoja na kuwajeruhi wengine wanane

  • | Citizen TV
    803 views

    Mtoto wa miaka 9 alifariki kufuatia ajali ya barabarani iliyotokea katika eneo la Ngata kwenye barabara kuu ya Nakuru - Kisumu. Watu wengine 8 walijeruhiwa kwenye ajali hiyo na kupelekwa hospitalini kwa matibabu. Maafisa wa usalama Nakuru mjini magharibi kwa sasa wanamzuulia dereva wa trela linaloaminika kusababisha ajali hiyo.