Ajira mitandaoni

  • | KBC Video
    16 views

    Vijana wamehimizwa kukumbatia teknolojia na kutumia mitandao ya kijamii kutekeleza biashara na kuimarisha ufanzaji. Akiongea kwenye uzinduzi wa kundi la wajasiriamali chipukizi, mkewe waziri mwenye mamlaka makuu, Tessie Musalia aliwahimiza vijana kutumia fursa ya kuwepo kwa vituo vya huduma za mtandao vilivyobuniwa na serikali katika maeneo bunge kushughulikia tatizo la ukosefu wa ajira.Aidha, Tessie aliwataka vijana kuipa serikali muda wa kushughulikia changamoto zinazowasibu. Naye naibu gavana wa kaunti ya Nakuru, David Jones alidokeza kuwa serikali ya kaunti hiyo imebuni vituo kadhaa vya kukuza talanta miongoni mwa vijana.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive