'Alikuwa kama ua la waridi na wakamuua'

  • | BBC Swahili
    1,168 views
    Wazazi wa watoto wa Palestina waliouawa wanataka haki itendeke kutokana na mauaji ya watoto wao yaliyofanywa na wanajeshi wa Israel katika Ukingo wa Magharibi Eneo linalokaliwa kimabavu. Umoja wa Mataifa wanasema ghasia zilizofanywa na Waisraeli wanaoishi katika eneo la Ukingo wa Magharibi kinyume cha sheria na utumiaji nguvu kupita kiasi wa jeshi la Israel umesababisha vifo vya Wapalestina 150 ambapo 33 kati yao ni watoto kwa mwaka 2022. Hii ni idadi kubwa zaidi tangu 2005 Umoja wa Mataifa ulipoanza kuweka kumbukumbu za mauaji #bbcswahili #israel #palestina