Aliyekuwa gavana wa Murang’a Mwangi Wa Iria asakwa na maafisa wa EACC

  • | Citizen TV
    3,573 views

    Aliyekuwa gavana wa Murang’a Mwangi wa Iria anasakwa na maafisa wa kupambana na ufisadi nchini EACC kwa tuhuma za ufisadi wa shilingi milioni 140 alipokuwa ofisini. Wa Iria aliponea kukamatwa kwenye hafla aliyopaswa kuhudhuria eneo la Magharibi ya Kenya. Wa Iria anasakwa pamoja na wengine saba kufuatia kufuatia idhini ya kufunguliwa kwake mashtaka na ofisi ya mkurugenzi wa mashtaka ya umma. Tuhuma hizi zinahusiana na ununuzi uliofanywa kati ya mwaka 2015 na 2016. Viongozi wa Azimio waliokuwa kwenye hafla ambayo wa Iria alipaniwa kuhudhuria walilaumu kile wanasema ni serikali kuwahangaisha viongozi wa upinzani