Aliyekuwa Waziri wa Elimu profesa George Magoha kuzikwa tarehe 11 mwezi wa Februari

  • | Citizen TV
    1,006 views

    Aliyekuwa Waziri wa Elimu profesa George Magoha atazikwa tarehe 11 mwezi huu wa Februari. Kulingana na aliyekuwa katibu wa Elimu ya msingi Julius Jwan ambaye anasimamia kamati yamazishi ya mwendazake, Ibada ya wafu itafanyika tarehe 9 katika kanisa la katoliki la Consolata mtaani Westlands jijini Nairobi kabla ya mwili wa marehemu kusafirishwa kuelekea Yala katika kaunti ya Siaya kwa mazishi yake katika kijiji cha Umiru. Magoha alifariki tarehe 24 mwezi Januari kutokana na mshtuko wa moyo akiwa na uMri wa miaka 71.